Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ali Al-Khatib, Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Kishia, aliwasili katika mji mtukufu wa Najaf Ashraf ikiwa ni sehemu ya safari yake nchini Iraq.
Sheikh Ali Al-Khatib alikutana na baadhi ya Marajii wa kidini huko Najaf Ashraf, ili kuwafahamisha kuhusu maendeleo ya hali nchini Lebanon, hususan katika maeneo ya kusini, kutokana na kuendelea uvamizi wa Israel na mashambulizi yanayoendelea dhidi ya maeneo ya kusini mwa nchi hiyo.
Huko Baghdad, alikutana na Nouri Al-Maliki, Waziri Mkuu wa zamani wa Iraq, na kumweleza kuhusu hali halisi ya Lebanon. Katika mkutano huo, walijadili na kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya eneo na mtazamo wa hatua ijayo.
Al-Maliki alieleza wasiwasi wake kuhusu hatua inayokuja kutokana na mabadiliko ambayo eneo hilo linayashuhudia, hususan katika kipindi kilichosalia kuelekea uchaguzi wa Marekani na Israel. Aidha, alisisitiza utayari wake wa kutumia kila juhudi kwa ajili ya kuisaidia Lebanon kuvuka hatua hii, hasa wananchi wa maeneo ya kusini ambao wanakabiliwa na mashambulizi ya Kizayuni.
Sheikh Al-Khatib, akiwa katika makazi yake kwenye Kasri ya Wageni inayomilikiwa na Ofisi ya Rais wa Baraza la Mawaziri la Iraq, alikutana na Mohammad Kazem Al-Sadiq, Balozi wa Iran nchini Iraq, ambaye alihudhuria akiwa pamoja na ujumbe kutoka ubalozini. Katika mkutano huo, walijadiliana kuhusu masuala ya Lebanon na eneo.
Pia alikutana na Naibu Mwenyekiti wa zamani wa Baraza la Wawakilishi la Iraq na Mwenyekiti wa Muungano wa Kibunge wa “Al-Asas”, Mbunge Mohsen Al-Mandalawi, ambapo walijadili masuala ya Lebanon, Iraq na maendeleo ya hali katika eneo.
Sheikh Ali Al-Khatib, Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Kishia, aliendelea na mikutano yake mjini Baghdad na viongozi wa Iraq baada ya kukutana na Waziri Mkuu Ali Falih Al-Zaidi.
Katika muktadha huo huo, Sheikh Al-Khatib alikutana kwa mfululizo na Sayyid Ammar Al-Hakim, Mwenyekiti wa Harakati ya “Al-Hikma”; Sheikh Qais Al-Khazali, Mwenyekiti wa Kundi la Kibunge la “Al-Sadiqoun”; Adil Abdul-Mahdi, Waziri Mkuu wa zamani wa Iraq; na Hadi Al-Amiri, Katibu Mkuu wa Shirika la Badr na Mbunge.
Katika mikutano hiyo, Sheikh Al-Khatib alifafanua hali ya sasa nchini Lebanon, hususan katika maeneo ya kusini, na kusisitiza: Watu wetu wanaishi ndani ya duara la hatari kutokana na mashambulizi yanayoendelea ya “Israel”; kiasi kwamba wavamizi wanaendelea na operesheni za kubomoa na kulipua maeneo yanayokaliwa kwa mabavu, jambo ambalo limewalazimisha wakazi wake—ambao idadi yao inafikia takribani 250,000—kuwa wakimbizi.
Wakimbizi hao wanaishi katika mazingira magumu sana ya maisha nje ya miji na vijiji vyao.
Maoni yako